Wenger na Mourinho warushiana maneno

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Arsene Wenger

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho amemjibu mwenzake wa Arsenal Arsene Wenger baada ya Wenger kuhoji kuhusu mbinu inayotumiwa na Chelsea kulinda lango lake.

Wenger alimchokoza kocha huyo wa Chelsea akisema kuwa ni rahisi kulinda lango,swala lililomshinikiza Mourinho kumjibu akisema kuwa iwapo kulinda lango ni rahisi ni kwa nini Arsenal walibanduliwa katika michuano ya kufuzu kwa robo fainali walipolazwa 3-1 na Monaco.

Timu hizo mbili zitakutana katika mechi ya ligi ya Uingereza itakayochezwa katika uwanja wa Emirates siku ya jumapili.