Mayweather:Mimi ni bora kuliko Moh'd Ali

Haki miliki ya picha AP
Image caption Mayweather

Floyd Mayweather amesisitiza kuwa yeye ndio bondia bora zaidi kuliko Mohammed Ali.

Ijapokuwa amesema kuwa anaheshimu kile kilichochangiwa na Ali katika mchezo wa ndondi,anasema kuwa amefanya zaidi ya Ali kwa kupigana bila kushindwa.

Mayweather alisema kuwa yeye ni bora kushinda Mohammed Ali,Sugar Ray kufuatia rekodi yake ya mapigano 47 bila ya kupoteza hata pigano moja.

Vilevile ameongezea kuwa hangeweza kushindwa na Leon Spinks aliyemshinda Mohammed Ali mwaka wa 1978.