Mabondia waalikwa Zambia na Serbia

Image caption Mabondia wa Tanzania wakioneshana kazi.

Mabondia wa Tanzania wamealikwa nchini Zambia na Serbia kushiriki michuano maalumu kwa ajili ya kujiiandaa na Michezo ya Afrika itakayofanyika nchini Congo Brazzaville kuanzia Septemba 4-19 mwaka huu.

Nchi mbalimbali zikiwemo Kenya na Uganda zinategemewa kushiriki huku maandalizi yakiwa yamepamba moto

Katibu mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema wanategemea kwenda Zambia kati kati ya mwezi ujao na Serbia mapema mwezi July.

Amesema michuano hiyo itasaidia kuwaandaa mabondia hapo ili wafanye vizuri nchini Congo.

“Ni matumaini yetu, kupitia michuano ya Zambia na Serbia, wachezaji wetu watakuwa wamejiandaa vema”, amesema Mashaga.

Image caption masumbwi ya kilo

Mbali na michezo ya Afrika, pia watatumia fursa za mashindano hayo kujiandaa na mashindano ya Dunia (AIBA World Boxing Championships) yatakayofanyika kuanzia Octoba 5-18 Doha, Qatar.

Mabondia wa Tanzania kwa sasa wanafanya mazoezi katika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi.

Mabondia hao ni Mohamed Mzeru, Maulid Athumani, Ibrahim Abdalah (uzito wa light- fly), Juma Ramadhani, Said Hofu, (uzito wa fly), Ahamad Furahisha, Bon Mlingwa, Elias Mkomwa, Bosco Bakari (uzito wa bantam).,