Borussia Dortmund yatinga fainali

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Kikosi cha Borussia Dortmund

Borussia Dortmund imetinga Fainali ya Kombe la ujerumani (DFB-POKAL)baada ya kuwabwaga Mabingwa Watetezi Bayern Munich kwa Penati 2-0 kufuatia Sare ya Bao 1-1 katika Dakika 120 za mchezo uliopigwa Allianz Arena.

Borussia Dortmund itacheza na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine inayochezwa Leo kati ya Timu ya Daraja la 3 Arminia Bielefeld na Klabu ya VfL Wolfsburg.

Katika Nusu Fainali hii, Bayern walitangulia kufunga Bao la Dakika ya 29 la Robert Lewandowski na Dortmund kurudisha Dakika ya 75 kwa Bao la mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang.

Katika Dakika za Nyongeza 30, Dortmund walibaki Mtu 10 baada ya Mchezaji wao Kampl kupewa Kadi Nyekundu lakini mwisho Bao zilibaki 1-1.

Kwenye Mikwaju Mitano ya Penati, Bayern walikosa Penati zao zote 4 zilizopigwa na Xabi Alonso, Philipp Lahm, Mario Gotze na Kipa Manuel Neuer huku Dortmund wakifunga 2 kupitia Sebastian Kehl na Ilkay Gundogan.