Helena Lucas achaguliwa- Uingereza

Image caption Helena Lucas bingwa wa mbio za boti akiwa amechaguliwa katika timu ya uingereza.

Bingwa wa mbio za meli kwa wachezaji wenye ulemavu (Paralympic )Helena Lucas amekuwa mchezaji wa kwanza kuchaguliwa katika timu ya Uingereza.

Mchezaji huyu ameitwa kwenye timu ya taifa kwa ajili ya michuano ya Olimpic ya Rio de Janeiro, itayofanyika mwezi August 2016 huku Brazil.

Michuano hii itakua ya tatu kwa Helena ambae alishiriki michuano ya keelboat kwa mchezaji mmoja mmoja. Baada ya uteuzi huu Helena afurahishwa na kushangazwa kuwa mchezaji wa kwanza kuteuliwa kwa ajili ya michezo ya olimpic.

Helena aliyezaliwa bila vidole gumba katika mikono yake alitwaa medali ya dhahabu mwaka 2012 na kuwa mchezaji wa kwanza wa Paralympic kutoka uingereza kutwa medali hiyo, tangu kuingiza rasmi kwa Paralympic katika michezo ya Olimpic mwaka 2000.