Tanzania kuchuana katika kuogelea Angola

Image caption Muogeleaji akiwa mazoezini

Timu ya taifa ya kuogelea ya Tanzania itashiriki michuano ya Kanda ya 4 itakayofanyika Luanda, Angola kuanzia Mei 6 hadi 9 mwaka huu.Michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya kufuzu kucheza Michezo ya Afrika itakayofanyika nchini Congo Brazzaville mwezi Septemba.

Sylivia Raphael, Smriti Gokarn, Collins Saliboko na Josephine Oosterhuis ni wachezaji waliochaguliwa na Chama cha mchezo huo (TSA).

Wachezaji hao kwa sasa wanafanya mazoezi ili kujiandaa vema na ushindani kutoka nchi nyingine ikiwemo Uganda.

Katibu mkuu wa TSA, Noel Kiunsi amesema wana imani wachezaji hao watafanya vizuri. Swimming umekuwa ni miongoni mwa michezo inayokuja juu nchini Tanzania huku wachezaji wake wakishiriki michuano mbalimbali kama vile ya Jumuiya ya Madola iliyofanyika Glasgow na michezo ya Olimpiki iliyofanyika London, Uingereza.