Tanzania itafanya vyema michuano ya pete

Image caption Wacheza mpira wa pete wakichuana.

Chama cha mpira wa pete nchini Tanzania (Chaneta) kimesema kina matumaini timu ya taifa itafanya vizuri katika michuano ijayo ya ya Afrika itakayofanyika Windhoek, Namibia June 8 mpaka July 5.

Mwenyekiti wa chama cha mpira wa pete ( netball) Tanzania Anna Kibira amesema wameamua kuanza mazoezi mapema ili kujiandaa na michuano hiyo mikubwa.

Wachezaji wa timu hiyo wamechaguliwa wakati wa mashindano ya Afrika ya Mashariki ambapo timu kutoka kutoka Kenya na Uganda zilishiriki mjini Zanzibar mwaka huu.

Kambi ya timu hiyo itafanyika Dar es Salaam.Timu hiyo kwa sasa ipo nafasi ya 15 katika viwango vya IFNA vya dunia na iliwahi kushinda kombe la Mataifa (Nations Cup) linalofanyika kila mwaka nchini Singapore huku timu kutoka Afrika zikialikwa. Uganda ndio bingwa wa kombe hilo kwa sasa, likichukua nafasi ya Tanzania.