McIlroy, Lee Westwood waibuka kidedea.

Image caption Rory Mcllory

Mchezaji namba moja wa Gofu Rory McIlroy na Billy Horschel wameibuka kidedea katika michuano ya Wgc.

Mcllroy alichakaza Brandt Snedeker na kuendeleza historia yake ya ushindi kwa asilimia mia.Huku Horschel akimfunga Jason Dufner, katika mchezo ulikua na msisimko.

kwa ushindi huu wametinga katika hatua ya kumi na sita bora ambayo itawakuanisha wachezaji waliofuzu kuanzia juzi.

Michezo ya leo Lee Westwood anahitaji ushindi dhidi ya Jordan Spieth ili kufuzu kwa raundi ya 16 bora.