Ugaidi:Shindano lasitishwa Ujerumani

Image caption Waendesha baiskeli

Polisi wa Ujerumani wamefuta mashindano ya kimataifa ya kuendesha baiskeli yaliyotarajiwa kufanyika ijumaa katika mji wa Frankfurt, kwa hofu ya shambulio la kigaidi.

Mume na mke wamekamatwa baada ya kupatikana na silaha katika makaazi yao ikiwemo kemikeli ya kutengeneza mabomu.

Polisi wanashuku kwamba wawili hao walikua na mpango, wa kufanya mashambulizi wakati wa mashindano ya kuendesha baiskeli ambayo yamevutia wachezaji wengi duniani.

Mwanamume na mwanamke wa miaka 30 walikua wakifuatwa na majasusi kwa majuma mawili baada ya kutumia majina bandia wakati wakinunua kemikali inayoweza kutengeneza mabomu.

Polisi waliamua kuvamia makaazi yao baada ya mwanamume mmoja anayeaminika kuwa na uhisiano na makundi ya kisiilamu yenye misimamo mikali kuonekana nje ya nyumba yao mara kadhaa.

Polisi walipata mabomba ya kutega mabomu, silaha na kemikali.

Haijabainika iwap wawili hao walikua wakishirikiana na mtandao fulani.