Mke wa Rio Ferdinand aaga dunia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Rio ferdinand

Mke wa aliyekuwa nahodha wa kikosi cha Manchester United pamoja na timu ya Uingereza Rio Ferdinand amefariki kutokana na saratani.

Mlinzi huyo wa kilabu ya QPR mwenye umri wa miaka 36 alitoa taarifa akisema mkewe mpendwa Rebecca Ellison aliaga dunia katika hospitali moja ya London.

Marehemu Elison mwenye umri wa miaka 34 aliyeoana na Ferdinand mwaka 2009 alikuwa akiugua saratani ya titi.

Image caption Rio Ferdinand na marehemu mkewe

Amewaacha watoto watatu.katika taarifa hiyo Ferdinand amesema kuwa mkewe alifariki ijumaa usiku.

''Rebecca,mkewe wangu alifariki baada ya kuugua kwa muda mfupi na saratani katika hospitali ya Royal Marsden mjini London'',alisema mchezaji huyo wa soka.