Liverpool yawika Everton yashindwa

Haki miliki ya picha Getty
Image caption nahodha wa Liverpool Steve Gerrard

Nahodha wa Liverpool Steve Gerrard alifunga bao la ushindi katika dakika za mwisho kwa upande wa Liverpool dhidi ya QPR ili kuweka matumaini ya Liverpool ya kufuzu kwa dimba la kilabu bingwa Ulaya msimu ujao.

Gerrard alifunga kichwa kizuru kufuatia krosi katika dakika ya 87 ikiwa mabao ni 1-1.

Phillipe Coutinho aliipatia Liverpool bao la kwanza kupitia mkwaju mzuri kabla ya Leroy Fer wa QPR kusawazisha.

Awali Gerrard alikosa mkwaju wa Penalti baada ya beki wa liverpool kuchezewa visivyo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Phillipe Coutinho

Wakati huohuo Christian Benteke alifunga mabao mawili na kuisadia Aston Villa kuicharaza Everton mabao matatu kwa mawili na hivyobasi kupanda hadi nafasi ya 14 katika jedwali la ligi.

Matokeo mengine ni

Leicester 3 - 0 Newcastle

Sunderland 2 - 1 Southampton

Swansea 2 - 0 Stoke

West Ham 1 - 0 Burnley