Manchester United yalazwa nyumbani

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Manchester United

Klabu ya manchester United ilishindwa kwa mara ya tatu mfululizo huku timu ya West Bromwich ikisongea juu ya jedwali la ligi ya Uingereza na hivyobasi kukwepa kushushwa katika ligi hiyo.

Manchester United ilitawala mechi lakini ikafungwa bao moja katikati ya kipindi cha pili baada ya mkwaju wa adhabu wa Chris Brunts kumgonga mchezaji mwenza Jonas Olson na kuingia wavuni.

Hatahivyo Manchester United ilitarajiwa kusawazisha baada ya kupata penalti lakini mkwaju huo wa mshambuliaji Robin Van Persie ulipanguliwa na kipa wa West Brom.Van Persie alikosa bao jingine baada ya kipa kuokoa mkwaju aliopiga.

Kwa sasa Manchester United iko juu ya Liverpool kwa pointi nne pekee katika nafasi ya nne.