Ligi kuu Tanzania kuendelea

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Azam Fc.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa kuendelea Jumatano kwa mchezo mmoja utakaopigwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, wenyeji timu ya Azam FC watawakaribisha Mabingwa wapya wa ligi hiyo msimu huu, timu ya Young Africans.

Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi wa kati Jacob Adongo kutoka Mara, akisaidiwa na washika vibendera Frednand Chacha (Mwanza), Hellen Mduma (Dar es Salaam), huku mwamuzi wa akiba akiwa ni Hussein Kalindo (Dsm) na Kamisaa wa mchezo huo ni Damian Mabena kutoka Tanga.

Hata hivyo, kwa Yanga, itakuwa ni kama kukamilisha ratiba wakati Azam wanahitaji ushindi katika vita yao ya Simba ya kugombania nafasi ya pili.

Bingwa, ambao ni Yanga watawaikilisha nchi katika michuano ya ligi ya mabingwa afrika wakati mshindi wa pili (kati ya Azam na Simba) wataiwakilisha nchi katika michuano ya kombe la Shirikisho.