Kikosi cha Taifa stars chatangazwa

Haki miliki ya picha bbc
Image caption Kocha wa Taifa Stars, Mart Nooij

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mart Nooij leo ametangaza kikosi cha wachezaji 28 .

Kikosi hicho kitaingia kambini katika hoteli ya Tansoma iliyo eneo la Gerezani jijini Dar es salaam, kujiandaa na michuano ya kombe la COSAFA na kuwania kufuzu kwa AFCON na CHAN mwezi Juni mwaka huu.

katika orodha hiyo ya wachezaji 28 watakaoripoti kambini jumatatu mchana, watapimwa afya zao na madakatari wa timu ya Taifa, na kisha watakaokuwa fit atachagua wachezaji 20 watakaokwenda kwenye michuano ya COSAFA nchini Afrika kusini.

Wachezaji walioitwa ni magolikipa: Deogratius Munish (Yanga), Aishi Manula, Mwadini Ali (Azam), walinzi: Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Nadir Haroub, Oscar Joshua, Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na Haji Mwinyi (KMKM).

Wengine ni viungo: Amri Kiemba, Salum Abubakar, Frank Domayo (Azam), Said Juma, Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba), Haroun Chanongo (Stand United) na Mwinyi Kazimoto (Al Markhira).

Washambuliaji ni Ibrahim Ajib (Simba), Mrisho Ngasa, Saimon Msuva (Yanga), John Bocco, Kelvin Friday (Azam) na Juma Luizio (Zeco United).

Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini siku ya jumatano, Mei 13 saa 1 jioni kwa shirika la ndege la Fastjet kuelekea nchini Afrika Kusini katika mji wa Rusterburg - North West Province ambapo ndipo michuano ya COSAFA CUP itafanyika kuanzia Mei 17 mpaka Mei 31 mwaka huu.