Tim Sherwood:'Benteke ndiye bora Ulaya'

Haki miliki ya picha PA
Image caption Benteke

Christian Benteke ndiyo mshambuliaji bora Ulaya kulingana na Kocha wa Aston Villa Tim Sherwood.

Mchezaji huyo wa miaka 24 aliyefunga bao saba katika mechi tano ameisaidia Villa kuondoka katika timu ambazo huenda zikashushwa daraja.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alikabidhiwa tuzo la mchezaji bora wa ligi ya Uingereza mwezi wa Aprili.

''Sidhani kama kuna mshambuliaji bora kwa sasa barani Ulaya'',''Benteke ndio bora zaidi''.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Benteke

Mkufunzi huyo wa Villa amesema kuwa hayuko tayari kumuuza nyota huyo wa Villa licha ya kuhusishwa na uhamisho wa Liverpool na Chelsea.

''Benteke haendi kokote mwisho wa msimu hu,u hakuna kilabu inayoweza gharama yake'',.aliongeza.