QPR yashushwa daraja baada ya kibano

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mancity yaibamiza QPR sita mtungi

Klabu ya QPR imeshushwa daraja kutoka ligi kuu ya Uingereza baada ya kucharazwa mabao sita bila na Manchester City.

Sergio Aguerro alifunga mabao matatu huku mabao yake mawili yakipatikana baada ya mabeki wa QPR kufanya masihara huku la tatu likipitia mkwaju wa penalti.

Aleksandr Kolarov alifunga kupitia mkwaju wa adhabu huku James Milner na David Silva wakipata mabao yao baadaye.

QPR ilihitaji ushindi wa mechi tatu zake za mwisho ili kuwa na fursa ya kusalia katika ligi kuu ,lakini kushindwa kwao na Mancity hakuridhishi.