La Liga:Matumaini ya R Madrid yadidimia

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Real madrid washangazwa na Valencia baada ya kutoka sare 2-2

Kilabu ya Real Madrid iligonga mwamba wa goli mara tatu huku nyota wake Christiano Ronaldo akikosa penalti na hivyobasi kupata sare ya 2-2 na timu ya Valencia hatua iliodidimiza matumaini yao kubeba taji la ligi hiyo.

Real ilitoka nyuma 2-0 na kupata sare hiyo na hivyobasi kuweka pengo la pointi nne kati yao na viongozi wa sasa Barcelona huku ikiwa imesalia mechi mbili.

Paco Alcacer aliipatia Valencia ilio nafasi ya nne katika jedwali uongozi kabla ya Javi Fuego kufunga la pili.

Mkwaju wa penalti uliopigwa na Ronaldo uliokolewa kabla ya Pepe kufunga bao la kwanza na Isco kuongeza bao la kusawazisha.Real Madrid pia ilipata pigo jingine baada ya kumpoteza Tony Kroos na jeraha katikati ya kipindi cha kwanza.