Afrika Mashariki yafuzu wavu ya ufukweni

Image caption Wachezaji wa mpira wa wavu ufukweni

Rwanda ndio mabingwa wa michuano ya mpira wa wavu wa ufukweni kwa wanawake yaliyofanyika katika Pwani ya Mombasa, nchini Kenya.

Michuano hiyo ilikuwa maalumu ili kupata timu zitakazofuzu kucheza Michezo ya Afrika nchini Congo Brazzaville kuanzia Septemba 4 mpaka 19.

Rwanda iliwafunga Kenya kwa seti 2-1 katika mechi ya kuamua bingwa . Wachezaji wa Kenya walioshindwa walikuwa Edna Rotich na Glaudencia Makokha wakati bendera ya Rwanda ilipeperushwa vema na Nosseir Mohammed na Elfayed Taufiq.Tanzania imefanya vibaya katika michuano hiyo na kushindwa kufuzu baada ya kupoteza mechi zake, ikiwemo ile kati yake na Uganda.

Kufanya vibaya kwa Tanzania kunazifanya timu nne za Rwanda, Rwanda, Kenya, Misri na Uganda kufuzu kucheza Michezo ya Afrika nchini Congo Brazzaville.