Carlo Ancelotti amkemea wakala wa Bale

Haki miliki ya picha AP
Image caption Carlo Ancelotti

Mkufunzi wa kilabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti amemtaka ajenti wa mchezaji Gareth Bale kufunga mdomo wake baada ya kusema kuwa wachezaji wenzake hawampigi pasii vya kutosha.

Jonathan Barnet amesema kuwa mshambuliaji huyo wa Wales anataabika kwa kuwa hapati usaidizi kutoka kwa wenzake.''Huu ni ulimwengu ambao watu wengi huzungumza na mara nyengine huzungumza kupitia kiasi'', alisema Ancelotti.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Gareth Bale

''Bale hajawahi kuwa na matatizo na wachezaji wenzake na wenzake pia hawajawahi kuwa na matatizo naye''.

Bale ndiye mchezaji aliye ghali mno baada ya kusajiliwa kwa kitita cha pauni miloni 85.3 kutoka klibu ya Tottenham katika ligi ya Uingereza mwaka 2013.