Andy Murry azidi kung'ara Italian Open

Haki miliki ya picha AP
Image caption Andy Murry

Kwenye mashindano ya Italian open, mcheza tenis Andy Murry amemrarua Jeremy Chardy kwa set 6-4 6-3 kwenye mchezo wa mzunguko wa pili. Kwa matokeo hayo Murry atamenyana na David Goffin kwenye mchezo utaopigwa baadae leo.

Kwa upande wake Heather Watson amegalazwa vibaya na Carla Suarez Navarro kwa set 6-1 6-1.