Juventus yaiangusha Real Madrid

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Juventus wakiruka hewani kwa raha zao

Katika hali isiyotarajiwa na wengi Juventus ya Italia imeingia fainali ya klabu bingwa barani Ulaya kwa jumla ya magoli 3 kwa 2 baada ya usiku wa kuamkia leo kutoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mechi ya mkondo wa pili dhidi Real Madrid ya Hispania. Madrid ndio walikuwa wa kwanza kuzifumania nyavu za wapinzani wao. Cristian Ronaldo alifunga goli hilo la kuongoza kwenye dakika ya 23 ya kipindi cha kwanza kwa mkwaju wa penati, lakini dakika ya 57 Alvaro Morata akaisawazishia Juventus.

Sasa ni waazi kwamba fainali ni Barcelona dhidi ya Juventus mchezo ambao utapigwa mjini Berlin Ujeruman mnamo June 6.

Mara ya mwisho Juventus ilitinga fainali za klabu bingwa mwaka 2003, walipocheza dhidi ya AC Milan.