Andre Schurrle aeleza hisia zake

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Andre Schurrle mchezaji wa zamani wa Chelsea

Mchezaji wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle amesema alipata mshangao kuona ujumbe mfupi wa maandishi kupitia simu ya kocha wake wa zamani Jose Mourinho ukisema medali ya ubingwa wa ligi kuu ilikuwa inamsubiri yeye.Schurrle amejiunga na Wolsburg kwa ya pound million 22 mnamo mwezi February.Katika msimu huu mchezaji huyo amecheza mara 14 tu katika mechi za mwanzoni na mara nyingi alikuwa akitokea benchi.“Mourinho alinitumia ujumbe kwenye simu kuniarifu kwamba nitapata medali na kunitaka niende katika mechi ya mwisho” alisema mchezaji huyo.“Sikujua kama ningepata medali kwakuwa sijacheza sana katika mkondo wa pili wa ligi” aliongeza Schurrle.