Kocha wa Simba arejea kwao

Image caption Kocha wa Simba Goran Kopunovic

Kocha wa Simba, Goran Kopunovic amerudi kwao Serbia na bado haijajulikana kama atarudi kuifundisha klabu hiyo.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya Simba, Zacharia Hans Pope amesema wana imani kocha huyo atarejea kuifundisha tena timu hiyo.

Kwa mujibu wa Hans Pope, Kopunovic anadai dau nono ili arudi kuendelea na kibarua, ilihali Simba haiwezi kutekeleza matakwa yake.

Kopunovic, aliyerithi mikoba ya aliyekuwa kocha wa klabu hiyo kutoka Zambia, Patrick Phiri, ameiwezesha Simba kumaliza nafasi ya tatu,

baada ya kuinasua kutoka katika nafasi za chini. Kocha huyo ameondoka na kuacha ripoti ya ushiriki wa timu katika ligi

na mapendekezo kadhaa, lakini hatima yake haijajulikana kufuatia kuisha kwa mkataba wake.

Habari zisizo rasmi kutoka Simba zinasema kuwa endapo kocha huyo hatakuwa tayari kukubaliana na uongozi, basi watalazimika kutafuta

kocha mwingine.