Taifa Stars yaanza kujifua kwa COSAFA

Image caption Kikosi cha timu ya Taifa Stars,Tanzania

Timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars inaendelea na mazoezi mepesi mjini Rustenburg, Afrika Kusini tayari kwa michuano ya Kombe la

COSAFA inayoanza Jumapili.Timu hiyo ilipokelewa vizuri na mashabiki na Watanzania waishio Afrika ya Kusini.

Michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya maandalizi ya Stars tayari kuivaa The Cranes ya Uganda katika mechi ya awali ya michuano ya CHAN (kwa

wachezaji wa ndani).

Kocha wa Stars, Mart Nooij amesema michuano hiyo itaiweka vema Stars kwa ajili ya CHAN na michuano ya AFCON ya 2017.

Michuano ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika viwanja vya Olympia Park na Moruleng, ikishirikisha

nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana zikiwa ni nchi waalikwa.

Nooij, kuelekea katika michuano hiyo, amewaacha wachezaji wanaocheza soka la kulipwa katika timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya watu wa

Congo, Mbwana Samatta na Thomasi Ulimwengu. Kikosi cha Stars kilichopo Afrika ya Kusini kinajumuisha wachezaji wafuatao.

Makipa: Deogratius Munish ‘Dida’ (Yanga) na Mwadini Ali (Azam), mabeki

ni Shomary Kapombe, Aggrey Morris, Erasto Nyoni (Azam), Oscar Joshua,

Kelvin Yondani (Yanga), Abdi Banda, Salim Mbonde (Mtibwa Sugar) na

Mwinyi Hajji Mngwali (KMKM).

Viungo; Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam), Said Juma,

Salum Telela, Hassan Dilunga (Yanga), Said Ndemla (Simba) na Mwinyi

Kazimoto (Al Markhiya, Qatar).

Washambuliaji ni Ibrahim Hajib (Simba), Mrisho Ngassa (Free State

Stars), Simon Msuva (Yanga), John Bocco (Azam FC) na Juma Luizio (Zeco

United).

Kutoka kulia Erasto Nyoni, Msuva, Shomary Kapombe na Hassan Dilunga