Boca Juniors nje ya Copa Libertadores

Haki miliki ya picha AP
Image caption Boca Juniors nje ya Copa Libertadores

Vigogo wa soka ya Argentina Boca Juniors wametupwa nje ya mchuano wa kombe la Copa Libertadores .

Boca walitupwa nje ya mashindano hayo baada ya mtafaruk kuibuka baina ya mashabiki wake na wale wa mahasidi wao wa jadi wa klabu ya River Plate katika mechi ya marudio iliyoandaliwa Alhamisi usiku.

Wachezaji wanne wa River Plate walilazimika kulazwa hospitalini katika tafrani hiyo ambayo ilishuhudiwa na mamilioni ya watazamaji kote kusini mwa Marekani.

Shirikisho linaloandaa mashindano hayo (Conmebol) lilikuwa limeipa Klabu hiyo ya Copa fursa ya kuthibitisha mashabiki waliotibua mechi hiyo katika kipindi cha pili hawakukuwa wake lakini wakashindwa.

Isitoshe Conmebol iliipiga klabu hiyo maarufu faini ya dola laki mbili mbali na kuamrisha wacheze mechi zao nne za nyumbani pasi na mashabiki.

Aidha Boca hawatakuwa na mashabiki katika mechi zingine nne za ugenini.

Licha ya hayo ushabiki sugu miongoni mwa vilabu hivyo viwili vilivyoko Buenos Aires hauoneshi dalili zozote za kufifia.

Tatizo lilianza baada ya mashabiki wabishi wa BOCA kupuliza pilipili katika kiingilio cha wachezaji wa River Plate.

Bila kujua wachezaji wa River Plate walianza kutatatizika pindi walipoingia uwanjani kwa kipindi cha pili wengi wao wakikimbilia chupa za maji ilikuosha macho yao ilikupunguza makali ya ya pilipili.

Haki miliki ya picha REUTERS
Image caption Tatizo lilianza baada ya mashabiki wabishi wa BOCA kupuliza pilipili katika kiingilio cha wachezaji wa River Plate.

Amini usiamini ulikuwa ni wakati mgumu kwao na wakaamua kukusanyika katikati mwa uwanja wa nyumbani wa Boca, Compact La Bombonera.

Maafisa wakuu walilazimika kusubiri kwa saa moja kabla ya kuchukua hatua ya kuahirisha mechi hiyo .

River Plate walikuwa wameshinda mkondo wa kwanza kwa bao moja kwa nunge kwa hivyo waandalizi wa mchuano huo waliamua kuwa River wangefuzu kwa mkondo unaofuatia.

River Plate sasa wameratibiwa kuchuana dhidi ya klabu ya Brazil Cruzeiro, katika hatua ya robo fainali.

Klabu hiyo ya Cruzeiro ilijikatia tikiti ya hatua hiyo baada ya kuilaza Sao Paulo kwa mikwaju ya penalti.