UEFA:Matumizi ya vilabu kuangaziwa

Haki miliki ya picha UEFA
Image caption UEFA

Shirikisho la soka barani Ulaya linajiandaa kuondoa sheria ya mwaka 2011 itakayozuia vilabu kufanya matumizi ya ziada.

Katika mahojiano na redio ya Ufaransa RTL,rais wa UEFA Michel Platini amesema kuwa sheria hiyo ilikuwa ikifanya kazi vizuri lakini itapigwa msasa mishoni mwa msimu huu.

Hatua hiyo inafuatia ripoti katika gazeti la Le Parisien siku ya jumapili iliosema kuwa kuna mabadiliko muhimu yatakayofanyiwa sheria hiyo.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Viongozi wa UEFA

Manchester City pamoja na kilabu ya PSG zilipigwa faini mwaka uliopita kwa kukiuka sheria hiyo.

Baadaye mwandani wa rais wa vilabu vya Ulaya ambaye pia ni katibu mpanga ratiba Gianni Infantino aliithibitishia BBC kwamba mazungumzo kuhusu FFP na vilabu vikuu vya Ulaya yanaendelea huku marekebisho hayo yakijadiliwa.