Liverpool:Sterling apata mtetezi

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mshambulizi wa Liverpool Raheem Sterling amepata mtetezi

Nyota wa Liverpool Raheem Sterling ametetewa kwa kuwa na hamu kujiunga na vilabu vikubwa.

Mshambuliaji huyo wa Liverpool huenda asilaumiwe kwa kuonyesha hamu ya kung'aa zaidi na kutaka kushinda vikombe.

Hii ni kwa mujibu wa mshambuliaji wa zamani wa Blackburn,Chris Sutton.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption "Je tunaweza kumlaumu Sterling kuwa na hamu ya kushinda vikombe?''aliuliza Sutton

Sterling mwenye umri wa miaka 20, anatarajia kumwambia meneja wa Liverpool Brendan Rodgers na mkurugenzi wa club hiyo Ian Ayre kuwa anataka kuihama Liverpool.

Tangu alipoanza kuonyesha nia yake yeye na wakala wake waliandamwa na kupingwa na wacheazaji wa zamani wa Liverpool.

"Sidhani kwamba uamuzi wake unahusu fedha" alisema Sutton

''Nahisi Sterling "anachotaka tu ni kujiunga na timu kubwa".

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Sterling anatarajiwa kuifahamisha Liverpool nia ya kuihama

Sutton aliihama Blackburn na kujiunga na Chelsea kwa pauni milioni 10 mwaka 1999.

"Je tunaweza kumlaumu Sterling kuwa na hamu ya kushinda vikombe?''aliuliza Sutton

"Liverpool ilishiriki mchuano wa ligi ya mabingwa mara moja tu katika kipindi cha miaka sita na kushinda kombe moja tu katika kipindi cha miaka tisa iliyopita."