Xavi kuihama Barcelona

Haki miliki ya picha AP
Image caption Xavi Hernandez

Wachezaji wa klabu ya Barcelona watavalia jezi maalum katika mechi yao ya mwisho msimu huu ili kutoa heshima kwa kiungo wao wa kati Xavi ambaye anakamilisha uhusiano wake wa miaka 24 na klabu hiyo .

Mchezaji huo atapewa kwaheri maalum katika mechi dhidi ya Deportivo la Coruna itakayochezwa katika uwanja wa Nou Camp siku ya jumamosi.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Xavi

Xavi mwenye umri wa miaka 35 ambaye atajishindia medali yake ya nane ya la liga alitangaza siku ya alhamisi kwamba ataondoka Barcelona mwishoni mwa msimu huu ili kujiunga na kilabu ya Qatar Al Saad.

Amesema kuwa uamuzi huo umekuwa mgumu kwake.