Roger Federer akosoa ulinzi Uwanjani

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Roger Federer akosoa ulinzi French Open

Mcheza tenis Roger Federer amekosoa ulinzi uliopo katika mashindano ya French Open baada ya mtazamaji mmoja kukimbilia uwanjani na kujaribu kupiga picha na mchezaji huyo raia wa Uswis.

Baadae mvamizi huyo aliondolewa, japo tayari alishafanikiwa kumuomba Federer akae mkao wa kupiga picha. "Sifurahii jambo hili, ilitokea pia wakati wa mazoezi ambapo mtoto mmoja alifika na kisha watatu zaidi wakaja"alisema Federer

Federer alipambana na kupata ushindi wa set 6-3 6-3 6-4 dhidi ya Mcolombia Alejandro Falla ambapo kijana mmoja alimsogelea wakati wakati yeye akiwa katika eneo la kuchezea.