Hamilton akumbwa na msongo wa mawazo

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Lewis Hamilton,ambaye kwa sasa anadaiwa kupata msongo wa mawazo baada ya kushindwa

Bosi wa timu ya Mercedes Toto Wolff ametanabaisha kuwa dereva wa timu hiyo Lewis Hamilton ataerejea katika hali yake ya kawaida baada ya kupata mfadhaiko uliotokana na matokeo mabaya katika mashindano ya Monaco Granda Prix.

Hamilton alijikuta akiangukia nafasi ya tatu mwishoni mwa wiki iliyopita japo kuwa anguko lake lilisababishwa na matatizo ya kiufundi katika gari alilokuwa analiendesha. ''ana hilo tatizo la msongo wa mawazo, na yupo katika harakati za kurejea kwenye hali yake ya kawaida. Inaumiza sana kupoteza mchezo ule kwa sababu ushindi ulikuwa wake, lakini sina shaka kwamba atarejea haraka kama afanyavyo siku zote" alisema bosi huyo. Mwenyewe Hamilton amesema hakuna wa kumlaum kwasababu wanafanya kazi kama timu. Kwenye ushindi huwa wote na kwenye kushindwa pia huwa wote.