Andy Murray kumvaa Joao Sousa,

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Andy Murray kupambana na Joao Sousa

Mashindano ya tenis ya French Open yanaendelea tena leo hii wakati waingireza wawili ,Andy Murray na Heather Watson wanashuka dimbani kucheza katika mzunguko wa pili.

Murry anatarajiwa kuvaana na Mreno Joao Sousa, wakati Watson atakwaana na Mmarekani Sloane Stephens. Wakati hayo yakijiri mchezaji Kyle Edmund ambaye ni raia wa Afrika kusini aliyezaliwa Uingereza, yeye amejiondoa katika mashindano hayo kabla ya kukutana na Nick Kyrgios kutoka Australia. Naye nyota nambari moja duniani katika tenis Novak Djokovic, Rafael Nadal na Serena Williams wapo katika mapambano kwa siku tano.