Andy Murray asonga mbele French Open

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Andy Murray asonga mbele mashindano ya French Open

Muingereza Andy Murray amezidi kusonga mbele katika mashindano ya French Open baada ya kutinga mzunguko wa tatu kwenye mashindano hayo pale alipomshinda Joao Sousa raia wa Ureno, kwa jumla ya set 6-2 4-6 6-4 6-1. Murry alianza mpambano huo akiwa vizuri na alibaki hivyo hadi mwisho, japo alionesha kupatwa na mshangao kutokana na ushindani mkali aliokutana nao kutoka kwa mpinzani wake huyo. Sasa Murray anataraji kuvaana na Nick Kyrgios kutoka Australia. "nilifurahi sana namna nilivyobadili mchezo na kuweza kufanya marekebisho pale uwanjani, ambapo upepo mzuri ukahamia kwangu" alisema Murray. Naye Muingereza mwingine Heather Watson, amegaragazwa na Mmarekani Sloane Stephens kwa set 6-2 6-4, huku Rafael Nadal na Novak Djokovic wakifanikiwa kusonga mbele kwenye hatua hiyo ya tatu.