Rio Ferdinand astaafu

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Aliyekuwa mlinzi wa timu ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand amestaafu kucheza kandanda ya kulipwa.

Aliyekuwa mlinzi wa timu ya Uingereza na Klabu ya Manchester United, Rio Ferdinand amestaafu kucheza kandanda ya kulipwa.

Ferdinand amesema kupitia kwa taarifa kwa meza ya michezo ya BT kuwa anahisi wakati umewadia kwake kufunganya virago na kushabikia mchezo anaoupenda.

Hatua hiyo ya mlinzi hiyo inafuatia kuruhusiwa kwake kuondoka na klabu ya Queens Park Rangers.

Klabu hiyo ya QPR ilimruhusu kuondoka baada ya kushushwa daraja baada ya kumaliza katika nafasi ya 20 katika ligi ya msimu huu iliyokamilika juma lililopita.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Ferdinand aliichezea Uingereza katika mechi 81

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 36 amesema ''nafikiri huu ndio wakati wa kustaafu kutoka kwenye mchezo ninaopenda''

''Lakini najivunia kuiwakilisha taifa langu katika mechi 81 za kimataifa''