FIFA yawapa marufuku maafisa wa soka Congo

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Fifa

Maafisa wawili wa shirikisho la soka nchini Congo Brazaville wamepigwa marufuku na shirikisho la soka duniani FIFA kwa ukiukaji wa maadili.

Makamu wa rais Jean Guy Blaise Mayolas na katibu mkuu Badji Mombo Wantete hawakubaliwi kushiriki katika maswala yoyote ya soka katika darafa la kitaifa na kimataifa.

Taarifa hiyo iliotolewa na FIFA imesema kuwa uamuzi huo ulichukuliwa baada ya wawili hao kukiuka kanuni na maadili ya FIFA.

Shirikisho hilo hatahivyo halikutoa maelezo zaidi kuhusu hatua yao.