Mo Farah ataka majibu kuhusu kocha wake

Haki miliki ya picha All Sport
Image caption Mo Farah

Mwanariadha Mo Farah wa Uingereza amekasirishwa na hatua ya kulitia jina lake katika matope na sasa anataka majibu kufuatia madai yanayomuhusisha kocha wake Alberto Salazar na dawa za kusisimua misuli.

Bingwa huyo wa Olimpiki kutoka Uingereza na vilevile bingwa wa dunia amesema kuwa atakuwa mtu wa kwanza kumuacha Salazar iwapo madai yaliotolewa na BBC ni ya kweli.

Haki miliki ya picha AP
Image caption Kocha wa Mo Farah Alberto Salazar

Chama cha riadha Uingereza hakina wasiwasi kwa wawili hao kufanya kazi pamoja.

Hakuna madai kwamba Farah amekiuka sheria na kwamba Salazar amekana madai yoyote ya kuhusika na dawa za kusisimua misuli.