Stanislas Wawrinka kidedea Ufaransa

Haki miliki ya picha reuters
Image caption Wawrinka akiwa na kombe lake alilolitwaa katika michuano ya French Open.

Stanislas Wawrinka atwaa ubingwa katika michuano ya wazi ya Ufaransa maarufu kama FRENCH OPEN

Wawrinka amefanikiwa kutwaa ubigwa wake wa kwanza wa michano ya wazi ya ufaransa kwa kumbwaga Novak Djokovic kwa seti 4-6 6-4 6-3 6-4 mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Roland Garros.

Nyota huyu wa tenesi mwenye miaka 30 alianza vibaya kwenye raundi ya kwanza kabla ya kurudi vizuri kuanzia raundi ya pili mpaka ya nne.

“Nataka nimshukuru kocha wangu Magnus Norman. Tulifika fainali mara mbili bila kushinda huu ni ushindi wake na wangu” alieleza mchezji huyo baada ya kumalika kwa mchezo huo

Ushindi huu unamfanya Wawrinka kuwa mchezaji wa kwanza wa urusi kushinda katika dimba la Roland Garros baada ya Roger Federer kuondosha katika nusu fainali.