Kombe la dunia ,England yaanza vibaya

Image caption Timu ya soka ya wanawake ya Ufaransa

Timu ya taifa ya wanawake ya England imeanza vibaya mashindano ya kombe dunia kwa upande wa wanawake yanayoendelea nchini Canada, kwa kukubali kipigo cha bao moja kwa yai viza kutoka kwa Ufaransa kwenye mtanange uliopigwa hapo jana.

Takriban dakika 29 tu za mchezo huo zilitosha kwa mwanadada Eugénie Le Sommer kupeleka msiba kwa timu ya England umbali wa yadi 20 tu.

Matokeo haya yanaendeleza ubabe wa taifa la Ufaransa kwa upande wa soka la wanawake, ambapo takribani miaka 41, England haijafanikiwa kuwashinda wapinzani wao hao.

Na katika viwanja vingine Hispania ilicheza dhidi ya Costa Rica,matokeo ni.moja moja.... Nayo Colombia ilivaana na Mexico, katika kipute hicho Colombia na Mexico nayo, moja moja. Na hatimaye Brazil walifumania nyavu mara mbili na korea ya kusini waliondoka kichwa chini.