Kombe la mataifa ya Afrika 2017

Image caption Taifa Stars ya Tanzania

Timu ya taifa ya Misri (Pharaohs) imeitumia salamu Taifa Stars ya Tanzania kwa ajili ya mechi yao ya kwanza ya kufuzu kucheza fainali za 2017 za AFCON baada ya kuwafunga Malawi 2-1 katika mechi ya kirafiki.

Taifa Stars itacheza na Misri mjini Alexandria Jumapili hii na kuelekea mchezo huo Stars imeweka kambi Addis Ababa, Ethiopia kwa ajili ya mechi hiyo ngumu. Mechi ya marudiano itachezwa Tanzania baada ya wiki mbili.

Licha ya ushindi huo, nahodha wa Stars, Nadir HAroub (Canavaro) amesema wamejipanga kuwakabili Misri licha ya kuwa timu tishio barani Afrika. Misri imeshinda taji la AFCON mara 7, wakati Stars haijawahi kushinda wala kufika hatua za mbali

Stars imepangwa kundi D pamoja na Super Eagle ya Nigeria na timu ya Chad.