Luis Enrique aongeza mkataba Barca

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Mwalimu wa timu ya Soka ya Barcelona,Luis Enrique

Mkufunzi wa timu ya soka ya Barcelona Luis Enrique ameongeza mkataba utakaomuweka klabuni hapo mpaka mwaka 2017

Katika Msimu wake wa kwanza tu akiwa na kikosi cha Barca, Enrique alimudu kutwaa makombe matatu baada kubeba Ubingwa wa La Liga, Copa del Rey na juzi kutwaa Kombe la klabu bingwa Ulaya.

Kocha huyu alikataa kueleza kama ataendelea kuwa kocha wa timu hiyo baada ya kumalizika kwa mchezo wa fainali ya klabu bigwa ulaya.

Rais wa Barca, Josep Maria Bartomeu, ndie alietangaza kuongezewa Mkataba Enrique huo mpya wa kocha huyo.

Enrique, ambae aliwahi kuzichezea Barca na Real Madrid, aliteuliwa Mwaka jana kuwa mbadala wa kocha Tata Martino amabe kwa sasa ni kocha wa timu ya taifa ya Ajentina.