Donaldo Ngoma kutua Yanga

Image caption Donaldo Dondo

Mshambuliaji wa Platinum FC ya Zimbabwe, Donaldo Ngoma anatarajiwa kuwasili Tanzania kwa ajili ya kukamilisha mazungumzo ya kujiunga na mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga.

Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Dar es Salaam muda wowote kuanzia sasa, kwa mujibu wa uongozi wa Yanga.

Yanga, wakiwa na kibarua cha kuiwakilisha Tanzania katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika mwakani, ipo katika nchakato wa kusajili wachezaji mahiri kwa ajili ya msimu ujao wa 2015/16 wa ligi kuu Tanzania Bara na michuano ya kimataifa. Hatua ya kujiimarisha inakuwa baada ya Yanga kutolewa katika ligi ya Kombe la Shirikisho mwaka huu na timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

Yanga ilivutiwa na Ngoma wakati ilipocheza na Platimun FC katika mechi za awali za Kombe la Shirikisho mwaka huu na kuitoa timu hiyo kutoka kusini mwa Afrika.