McClaren ndio kocha mpya wa Newcastle

Haki miliki ya picha z
Image caption McClaren

Steve McClaren ameajiriwa kuifunza klabu ya Newcastle United.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 54 anachukua mahala pake John Carver ambaye alipigwa kalamu siku ya jumapili na maneja huyo wa zamani wa Uingereza pia amewekwa katika bodi ya timu hiyo.

Mike Ashley amewacha wadhfa wake katika bodi lakini bado anasalia kuwa mwenyewe.

McClaren ambaye amepewa kandarasi ya miaka mitatu ambayo huenda ikaongezwa na kufika miaka minane alisema:''Nimejitolea kuwapatia mashabiki timu ambayo wataipenda''.

Kocha huyo wa zamani wa Uingereza ambaye alipigwa kalamu na klabu ya Derby mwezi Mei ,aliikataa kazi hiyo mara mbili baada ya Alan Perdew kuondoka na kabla ya kukamilika kwa mechi tatu za mwisho za msimu huu.