Zico Coimbra kuwania urais FIFA

Image caption Zico Coimbra,akitangaza nia

Huku kukiwa bado hali si shwari ndani ya shirikisho la soka Ulimwenguni FIFA, mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Brazil Zico amepania kugombea urais wa shirikisho hilo baada ya kukiri kufadhaishwa na janga la rushwa katika uongozi wa FIFA.

Zico mwenye miaka 52 na ambaye jina lake halisi ni Arthur Antunes Coimbra, amesema ni wajibu wake kugombea. Akizungumza na kundi kubwa la waandishi wa habari katika kituo chake cha kufundisha soka huko mjini Rio de Janerio, Zico amesema ni huzuni kwaenye michezo kuona kile kinachotokea katika soka leo hii.Kuona rushwa, lakini pia kuona uchapakazi unaofanywa na baadhi ya watu wazuri ukipotezwa.Pia aliongeza kuwa, ni wajibu wake sasa kutumiauzoefu na ujuzi wake kujaribu kugombea urais.

Hivi karibuni rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter, alitangaza kuwa atajiuzuru wadhfa wake huo ikiwa ni siku nne tu baada ya kuchaguliwa tena kushika madaraka hayo. Uamuzi huo wa Blatter ulikuja ikiwa ni siku chache tu baada mamlaka ya Marekani na Uswiz kufungua kesi ya rushwa ya kwa baadhi ya maafisa FIFA.