Floyd mwanamichezo anayelipwa zaidi

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Floyd Mayweather Jr, mwanamichezo anayelipwa zaidi ulimwenguni

Bondia Floyd Mayweather Jr ndio mwanamichezo aliyeingiza pesa nyingi zaidi dunia katika kipindi cha miezi 12 iliyopita kwa mujibu wa jarida la Forbes.

Mayweather ameingiza kiasi cha dola milioni 300 katika kipindi cha miezi hiyo na fedha nyingi ikiwa imepatikana kutoka na pambano lake na bondia Manny Pacquiao.

Manny ameshika nafasi ya pili katika orodha hiyo huku nyota wa kandanda Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya tatu kwa wanamichezo waliotengeneza pesa nyingi.

Orodha kamili ipitie katika tovuti ya bbcswahili.com

Ifuatayo ni orodha kamili ya wanamichezo hao

1. Floyd Mayweather, US, US$300m (£194m).

2. Manny Pacquiao, Philippines, $160m (£103.4m)

3. Cristiano Ronaldo, Portugal, $79.6m (£51.4m)

4. Lionel Messi, Argentina, $73.8m (£47.7m)

5. Roger Federer, Switzerland, $67m (£43.3m)

6. LeBron James, US, $64.8m (£41.9m)

7. Kevin Durant, US, $54.1m (£35m)

8. Phil Mickelson, US$50.8m (£32.8m)

9. Tiger Woods, US, $50.6m (£32.7m)

10. Kobe Bryant, US, = $49.5m (£32m)