Ombi la kumnunua Sterling lakataliwa

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Raheem Sterling

Liverpool imekataa ombi la kitita cha pauni milioni 25 na nyongeza ya pauni milioni 5 kutoka kwa Manchester City ili kumnunua Raheem Sterling.

Pia inaaminika kwamba Liverpool inamthamini mchezaji huyo wa miaka 20 kuwa na thamani ya pauni milioni 50 na kwamba haina mpango wa kumuuza .

Image caption mancity

Mchezaji huyo amehusishwa na mzozo katika uwanja wa Anfield na hivi majuzi alisema kuwa hatoweka sahihi ya mkataba mwengine katika klabu hiyo.

Hatahivyo ajenti wa Sterling Aidy Ward amedaiwa kusema kwamba hatokubali kandarasi nyengine katika klabu ya Liverpool hata akipewa kandarasi ya pauni laki tisa kwa wiki.