Adebayor kucheza kesho Liberia

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Adebayor kucheza kesho Liberia

Mshambulizi wa Togo Emmanuel Adebayor atacheza dhidi ya Liberia hapo kesho katika mechi ya mkondo wa kwanza ya kuwania nafasi ya kushiriki kombe la mabingwa barani Afrika.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 ameratibiwa kushambulia Liberia licha ya kuwasili kambini akiwa amechelewa.

Adebayor ambaye hakushiriki mechi ya kupimana nguvu baina ya Togo na Black Stars ya Ghana amekuwa na wakati mgumu kikosini baada ya kocha

Tom Saintfiet kumkashifu mshambulizi huyo wa klabu ya Uingereza ya Tottenham Hostpurs kwa kuwa mtundu.

Adebayor ameiambia dawati la michezo la BBC kuwa alichukua fursa ya kumweleza kocha Saintfiet

Haki miliki ya picha getty image
Image caption Togo imeratibiwa kuchuana na Liberia katika mechi ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika

kuwa mechi hiyo haikuwa na umuhimu wowote kwao na hivyo alikuwa radhi asiicheze .

Hata hivyo mshambuliaji huyo alisema kuwa ''Tofauti na mechi ya Ghana ,mechi hii ya hapo kesho dhidi ya Liberia inaumuhimu mkubwa sana kwetu.

Iwapo tunataka kufuzu kwa mkondo ujao wa kuwania nafasi ya kombe la mabingwa barani Afrika, hatuna budi ilakuishinda.''

Kocha Saintfiet amethibitisha kuwa Adebayor - Kossi Agassa na Floyd Ayite - watakuwa uwanjani katika mechi hiyo muhimu.