Brazil yaingia robo fainali Copa America

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Brazil waishinda Venezuela na kuingia robo fainali

Thiago Silva na Roberto Firmino walifunga bao moja kila mmoja na kuisaidia Brazil kujikatia nafasi ya kuingia katika robo fainali ya mchuano wa Copa America baada ya kuilambisha sakafu Venezuela.

Silva alifunga kona maridadi baada ya kupata pasi kutoka kwa Robinho huku akianza mechi hiyo kwa nafasi ya Neymar baada ya kupigwa marufuku katika michuano hiyo.

Awali Firmino aliipinda krosi ya Miku na kufunga bao la kufutia machozi.

Sasa Brazil itakwaruzana na Paraguay katika mchuano wa robo fainali mnamo siku ya Jumamosi.

Colombia na Peru pia zilifuzu baada ya kutoka sare tasa mapema mchana.

Katika michuano mingine ya robo fainali, Chile itavaana na Uruguay Ijumaa, Juni 25, Bolivia wavaane na Peru, huku Argentina wakikwaruzana na Colombia, ilihali Brazil itakung'utana