Man U yamwinda Schweinsteiger na Ramos

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Scweinsteiger

Klabu ya Manchester United ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Bastian Schweinsteiger na mlinzi wa Real Madrid Sergio Ramos.

Kocha wa klabu hiyo Louis Van Gaal anajaribu kuimarisha kikosi chake baada ya kumaliza katika nafasi nne katika jedwali la ligi ya EPL.

Haki miliki ya picha Getty
Image caption Sergio Ramos

Schweinsteiger mwenye umri wa miaka 30 na Ramos mwenye umri wa miaka 29 ni kati ya wale wanaomvutia.

Kandarasi ya Ramos itakamilika mwaka 2017 huku ile ya Schweinsteiger ikiendelea hadi mwisho wa mwaka 2016.