Wachezaji wa tenisi wawasili Tanzania

Image caption Mcheza tenisi akiwajibika uwanjani

Wachezaji wa mchezo wa tenisi, kutoka nchi za Kenya, Uganda, Rwanda, Zambia, Malawi wamewasili jijini Dar es Salaam, Tanzania kwa ajili ya michuano ya tenisi ya wazi kwa nchi za ukanda wa Afrika ya Mashariki.

Michuano hiyo, inayojulikana kama “Acacia Open”, inategemewa kuanza Jumatano katika viwanja vya Gymkhana.

Baadhi ya wachezaji wamewasili Jumatatu na wengine wanawasili Jumanne kwa ajili ya michuano hiyo. Ratiba kwa ajili ya michuano hiyo inapangwa Jumanne baada ya wachezaji wote kuwasili.

Tanzania imekuwa mwenyeji wa michuano mbalimbali ya tenisi, yakiwemo yale ya ITF kwa nchi za Afrika ya Mashariki na Kati.