Italia yainyuka England

Image caption Timu ya Italia ikishangilia bao.

Timu ya England chini ya miaka 21 imekubali kichapo cha Mabao 3-1 kutoka kwa Italia katika michuano ya ulaya.

Italia walianza kuandika bao lao la kwanza dakika ya 25 ya mchezo, kwa bao la Andrea Belotti Kabla ya Marco Benassi kuongeza mengine mawili dakika ya 27 na 72.

Nathan Redmond akaifungia timu yake ya England bao la kufutia machozi baada ya kazi nzuri liliyofanya na kiungo Ruben Loftus-Cheek.

Katika mchezo mwingine wa michuano hii Ureno walikwenda sare ya kufungana bao 1-1 na sweden.

Kwa matokea haya Ureno na sweden wanasonga mbele kenye hatua ya Nusu fainali na kuungana na mataifa ya Ujeruman na Denmark.