Konta asonga mbele Watson atupwa nje

Image caption Johanna Konta akifurahia ushindi

Mcheza tenesi Johanna Konta ametinga hatua ya nane bora ya michuano ya kimataifa ya tenesi ya Aegon.

Konta anayeshika nafasi ya 146 kwa ubora duniani amemfunga mpinzani wake Garbine Muguruza wa Hispania anayeshikilia nafasi ya 14 kwa ubora wa dunia kwa jumla ya seti 6-4 4-6 6-3.

Ushindi huu wa nyota huyu wa tenesi unakuja ikiwa nia saa 24 tangu alipomfunga nyota namba nane Ekaterina Makarova, na kuwa ushindi wake wa kwanza dhidi ya wachezaji walioko kwenye 20 bora.

Konta atachuana na Belinda Bencic katika hatua ya nane bora.

Huku nyota mwingine wa tenesi wa Uingereza Heather Watson ametupwa nje kwenye michuano hiyo baada ya kugalagazwa na Sloane Stephens, kwa seti 6-26-3 katika mchezo uliotumia saa 1 na dakika 16.